CEO wa Simba, Barabara atangaza kujiuzulu

0
734

Barbara Gonzalez ametangaza kujiuzulu wadhifa wa Mkurugenzi Mtendaji wa Simba SC kuanzia Januari 2023 ili kutoa nafasi kwa bodi ya wakurugenzi itakayochaguliwa kupata nafasi ya kuchagua mtendaji mkuu na menejimenti mpya.

Aidha, sababu nyingine aliyoitoa ni kujipa nafasi ya kutimiza fursa nyingine kwingineko.

Katika barua aliyoichapisha kwenye ukurasa wake wa Instagram amewashukuru wote aliofanya nao kazi na kuifanya Simba SC kuzidi kuwa kubwa.

“Ni uamuzi mgumu sana kuiacha kazi unayoipenda na ulioifanya kwa moyo wote, lakini ni kweli kwamba mambo yote mazuri huwa na mwisho,” ameandika Barbara.

Katika kipindi cha uongozi wake Simba imepata mafanikio mbalimbali ndani na nje ya uwanja ikiwa ni pamoja na kutwaa mataji, kuvutia wafadhili na kuendelea kuheshimika kama moja ya klabu kubwa Afrika.