Zidane akataa kurejea Real Madrid

0
416

Rais wa zamani wa timu ya Real Madrid ya nchini Hispania, -Ramon Calderon amesema kuwa kocha wa zamani wa timu hiyo Zinedine Zidane amekataa ofa ya kurejea tena kwenye timu hiyo ili kuioko kutoka kwenye hali ngumu iliyonayo hivi sasa hasa baada ya kutolewa kwenye michuano ya Ulaya na Ajax Amstadam.

Zidane mwenye umri wa miaka 46 aliondoka kwenye timu hiyo siku Tano baada ya kuiongoza kutwaa  mara tatu mfululizo ubingwa wa Ulaya mwezi Mei mwaka 2018 ambapo Real Madrid iliifunga Liverpool kwenye fainali.

Calderon amesema kuwa Rais wa sasa wa timu hiyo ya Real Madrid, -Florentino Perez alimpigia simu Zinedine Zidane ili kumuomba arejee kwenye timu hiyo lakini kocha huyo Mfaransa mwenye asili ya Algeria almekataa ofa hiyo.

Zidane aliwashangaza wengi kwa kuicha Real Madrid kutokana na mafanikio aliyoyapata ambapo aliingia kwenye historia ya kuwa kocha wa kwanza kuiongoza timu kutwa taji la Ulaya mara tatu mfululizo na ni kocha wa tatu kutwaa taji hilo mara tatu akitanguliwa na Bob Paisley na Carlo Ancelotti.

Tangu aondoke Real Madrid hadi hivi sasa,  Zinedine Zidane hana kazi na siku za hivi karibuni alihusishwa na kwenda kuifundisha timu ya Chelsea ya nchini England.