Rais Donald Trump wa Marekani amesema kuwa amesikitishwa kupata taarifa kuwa kiongozi mwenzake wa Korea Kaskazini, – Kim Jong Un ameanza tena kufufua vinu vyake vya nyuklia alivyotangaza kuwa ameviteketeza.
Trump amesema kuwa anafuatilia suala hilo kwa karibu ili kujua ukweli, kwani mazungumzo kati yake na Un yaliyofanyika nchini Vietnam yalikwenda vizuri, licha ya kutofautiana katika mambo kadhaa yaliyosababisha kuondoka kwenye chumba cha mazungumzo.
Rais huyo wa Marekani aliondoka kwenye chumba cha mazungumzo kati yake na Un, kwa madai ya kutoridhiwa na masuala kadhaa yaliyowasilishwa kwenye mkutano huo.