Vijana nchini wametakiwa kujivunia lugha ya Kiswahili popote wanapokuwa, kwani kwa sasa lugha hiyo inazungumzwa na watu wengi zaidi duniani.
Hayo yamesemwa na Gervas Kisaga, Mhadhiri Idara ya Kiswahili Chuo Kikuu Dodoma, wakati akichangia mada kwenye kongamano la Kiswahili la miaka 61 ya Uhuru.
Amesema lugha ya Kiswahili imekuwa na mchango mkubwa katika kukuza sanaa na katika kuelimisha masuala mbalimbali ndani na nje ya nchi.