Rais Kagame aanza ziara nchini

0
504

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Rais Paul Kagame wa Rwanda amewasili nchini kwa ziara ya kikazi ya siku mbili.

Katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam, Rais Kagame amepokelewa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Profesa Palamagamba Kabudi na viongozi wengine mbalimbali.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ziara ya Rais Kagame inafuatia mwaliko wa Rais John Magufuli.

Viongozi hao wawili wanatarajiwa kujadili masuala mbalimbali kuhusu uhusiano na ushirikiano baina ya Tanzania na Rwanda na pia watazungumzia masuala yanayohusu mtangamano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki.