Kiswahili chapaa kimataifa

0
51

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Consolata Mushi amesema lugha ya kiswahili inaendelea kukua na kuenea kwa kasi katika mataifa mbalimbali, ambapo zaidi ya watu milioni mia tano duniani wanazidi kujifunza na kutumia lugha hiyo katika shughuli mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

Consolata amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa kongamano la Kiswahili la miaka 61 ya Uhuru.

Amesema lugha ya Kiswahili inazidi kupendwa na kuzungumzwa na watu wengi ndani na nje ya Bara la Afrika.