Clouds waomboleza kifo cha Kibonde

0
410

Taarifa mbalimbali zinaendelea kutolewa kufuatia kifo cha Mtangazaji maarufu wa Clouds Media Group, – Ephraim Kibonde kilichotokea alfajiri ya leo mkoani Mwanza baada ya kuugua ghafla.


Mganga Mkuu wa mkoa wa Mwanza Dkt Thomas Rutachunzibwa amesema kuwa, Kibonde amefariki dunia akiwa njiani kuhamishiwa hospitali ya Bugando akitokea hospitali ya Uhuru mkoani humo.


Baadhi ya Wafanyakazi wa Clouds Media Group wamesema kuwa, Kibonde alianza kuugua wakati wa msiba wa Ruge Mutahaba aliyekua Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji wa Clouds ambaye mazishi yake yamefanyika Jumatatu wiki hii mkoani Kagera.


Kibonde atakumbukwa kwa utangazaji wake uliojaa ucheshi na mzaha hasa katika kipindi cha Jahazi kinachotangazwa na Redio Clouds.