Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Atashasta Nditiye ametoa wito kwa wananchi kutumia mitandao kujiletea maendeleo badala ya kutumia mitandao ya simu ya internet katika kufanya uhalifu.
Akifunga mkutano wa baraza la uongozi wa taasisi ya mawasiliano kwa nchi za Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika -Afralti Waziri Nditiye amesema serikali imejipanga vema kiteknolojia kukabiliana na uhalifu wa mtandaoni.