Majangili wabwaga manyanga

0
990

Watu 30 waliokuwa wanajihusisha na ujangili katika mapori ya akiba ya Kijereshi na Maswa pamoja na hifadhi ya taifa ya Serengeti wameamua kuachana na ujangili baada ya shirika linalojihusisha na uhifadhi la Peace for Conservation kuwaelimisha kuhusu madhara ya ujangili.

Mkurugenzi wa shirika hilo Leonard Kabambo na Meneja wa pori la akiba la Kijereshi Diana Kachambi wamesema watu hao ambao hivi sasa wanatumika kuielimisha jamii athari za ujangili wamesaidia kupunguza vitendo vya ujangili.