Dkt Mwinyi kuiwezesha CCM kiutendaji

0
119

Makamu Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa upande wa Zanzibar Dkt. Hussen Mwinyi amesema dhamira yake ni kukiwezesha chama hicho ili kiweze kuongeza kasi katika utendaji wake.

Dkt Mwinyi amesema hayo mkoani Dodoma wakati wa mkutano mkuu wa 10 wa chama hicho ambapo amesisitiza suala la kasi zaidi katika utekelezaji wa miradi mbalimbali inayosimamiwa na CCM.

Dkt Mwinyi ambaye pia ni Rais wa Zanzibar amesema kuwa, Chama Cha Mapinduzi kina rasilimali nyingi lakini bado hazijatumika vema, hivyo ni muhimu zikatumika vema ili kuendelea kukiboresha chama hicho.