Wanaofanya udanganyifu kwenye mitihani kushughulikiwa

0
66

Serikali imetangaza kuwachukua hatua kali maafisa elimu wa mikoa, wilaya, walimu na maafisa wengine ambao wamepewa jukumu la kusimamia mitihani na kufanya udanyanyifu katika mtihani hiyo.

Hatua hizo ni pamoja na kuwasimamisha kazi, kuwafukuza kazi na kuwafikishaa mahakamani ili sheria ichukue mkondo wake.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda ameyasema hayo mkoani Dar es Salaam, alipokuwa akizungumza na uongozi wa chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili kampasi ya Mlongazila alipofanya ziara ya kikazi ya siku moja.

Amesema ili kuimarisha sekta ya elimu nchini ni lazima kuwashughulikia watu wanaofanya udanganyifu ikiwemo kuwachukulia hatua kali na sio tu kuwafukuzwa kazi kama ilivyozoeleka au kupewa onyo pekee bali kuwafunga gerezani ili iwe fundisho kwa wengine.

“Sasa nisisitize kuna kauli inasema ukitaka kuua Taifa basi uwa elimu, sasa tunafanya mageuzi ya elimu nchini kwenye sera na mitaala lakini haiondoi jukumu la kusimamia elimu tunayoitoa sasa hivi inatolewa kwa taratibu zinazokubalika.” amesisitiza Waziri Mkenda