Faru weupe kupelekwa Burigi Chato

0
107

Shirika la Hifadhi za Taifa (TANAPA) limeiteua Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato kuwa kati ya hifadhi mbili nchini zitakazoendeleza na kukuza Faru weupe ambao hawapo katika hifadhi nyingi hapa nchini.

Kupelekwa kwa Faru hao weupe katika hifadhi hiyo ambayo ni ya tano kwa ukubwa kati ya hifadhi 22 nchini, kutaifanya kuwa miongoni mwa hifadhi za Taifa zenye sifa ya kuwa na wanyama wakubwa watano.

Msimamizi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi Chato
Kamishna Msaidizi wa Uhifadhi John Nyamhanga amesema, kupelekwa kwa Faru weupe katika hifadhi hiyo kitakuwa ni kichocheo kikubwa cha kuvutia watalii.