Afua ya upimaji VVU yaonyesha mafanikio

0
48

Katika kuendeleza mapambano dhidi Ukimwi nchini, Afua ya upimaji imetajwa kuwa ni moja kati ya afua ambazo zinaonyesha mafanikio makubwa katika mapambano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukiwmi Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Redempta Mbatia amesema, asilimia 99 ya watu wote waliopima na kugundulika kuwa na virusi vya Ukimwi walianza kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo.

Kwa upande wao wanufaika wa THPS wamesema, kupitia shirika hilo wamepata elimu kuhusu virusi vya Ukimwi na kuamua kutambua hali za afya zao, na ambao wamegundulika wana virusi hivyo wameanza kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo.

Watu 1,353 kati ya 13,764 waliopima virusi vya Ukimwi kupitia taasisi ya Tanzania Health Promotion Support wameanza kutumia dawa za kufubaza virusi hivyo baada ya kujigundua wameambukizwa virusi vya Ukimwi.

Watu hao wameanza kutumia dawa hizo kupitia ufadhili wa Centers For Disease Centrol (CDC), PEPFAR na USAID.

Katika kuendeleza mapambano dhidi Ukimwi nchini, Afua ya upimaji imetajwa kuwa ni moja kati ya afua ambazo zinaonyesha mafanikio makubwa katika mapambano hayo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Lindi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Siku ya Ukimwi Duniani, Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Redempta Mbatia amesema, asilimia 99 ya watu wote waliopima na kugundulika kuwa na virusi vya Ukimwi walianza kutumia dawa za kufubaza makali ya virusi hivyo.