IGP Nigeria kwenda gerezani miezi 3

0
307

Mahakama Kuu nchini Nigeria imemhukumu kifungo cha miezi mitatu gerezani Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini humo Usman Alkali Baba kwa kutotii amri ya mahakama hiyo.

Uamuzi huo wa Mahakama Kuu umefuatia sakata la kesi ya afisa mmoja wa polisi nchini humo ambaye alipinga mahakamani hatua ya kufukuzwa kazi mwaka 1992, ambapo mahakama hiyo iliamuru arejeshwe kazini.

IGP Usman Alkali Baba anatakiwa kutumikia kifungo hicho cha miezi mitatu gerezani au kutii amri ya Mahakama Kuu ya kumrejesha kazini afisa huyo wa polisi.

Habari zaidi kutoa nchini Nigeria zinaeleza kuwa mpaka sasa Jeshi la Polisi nchini humo limeshindwa kutekeleza agizo hilo, huku likisema uamuzi huo wa Mahakama Kuu wa kumuhukumu IGP kifungo cha
miezi mitatu gerezani ni wa kushangaza.

Limesema linasoma hukumu hiyo ili kujua hatua za kuchukua.