Majaliwa: Vyanzo vipya vya maji vitafutwe

0
42

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) kuendelea kutafuta vyanzo vipya vya maji na kuviingiza kwenye mfumo.

Amesema licha ya kuongezeka kwa kiwango cha maji kwenye mfumo wa uzalishaji na usambazaji, wasilale bali waendelee kuwatumia wataalam wa ndani kutafuta maji zaidi.

Waziri Mkuu Majaliwa ameyasema hayo alipotembelea eneo la mradi wa maji Kisarawe mjini, mkoani Pwani.

Pia Waziri Mkuu Majaliwa amesema kumekuwa na ongezeko la makazi, viwanda na shughuli mbalimbali za kujamii ambazo kwa kiasi kikubwa zinahitaji uwepo wa maji ya kutosha.

“Tusilale tuendelee na uzalishaji wa maji, tunataka huduma hii isambae na iwafikie watu wote.” amesema Waziri Majaliwa na kuongeza kuwa

“Ndugu wafanyakazi wa DAWASA mnapaswa kutambua maji ni huduma nyeti kwenye maisha ya binadamu, kazi yenu inahitaji uaminifu na uadilifu mkubwa, fanyeni kazi hii ya umma, wahudumieni watanzania, tambueni maeneo yenye uhitaji na mpeleke huduma.”