Mtwara watakiwa kujitokeza kumpokea Rais

0
49

Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Kanali Ahmed Abbas amewataka wananchi mkoa huo kujitokeza kwa wingi kumpokea Rais Samia Suluhu Hassan ambaye anatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Mtwara Desemba Mosi mwaka huu, akielekea mkoani Lindi kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya Ukimwi Duniani yatakayofanyika kitaifa mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani Mtwara Kanali Abbas amewahimiza wakazi wa Mtwara kujitokeza tarehe hiyo kuanzia saa 12 asubuhi, ili kumlaki na kusalimiana na Rais Samia Suluhu Hassan katika maeneo ya nje ya uwanja wa ndege, shule ya sekondari ya wasichana ya Mtwara, barabara kuu ya kuelekea Lindi, Magomeni na Mkanaledi.