Chatanda : Maendeleo ya wanawake lazima

0
45

Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Wanawake Tanzania ( UWT) Mary
Chatanda, ameahidi kushirikiana na wanachama wote wa Jumuiya hiyo pamoja na wanawake wote wa Tanzania ili kuleta maendeleo ya wanawake wote.

Chatanda ametoa kauli hiyo mkoani Dodoma wakati akiwashukuru wajumbe wa mkutano mkuu wa 10 wa UWT waliompigia kura za ndio na hata wale ambao hawakumpigia kura.

Amesema Wanawake wa Tanzania wanafanya jitihada kubwa za kujiletea maendeleo, hivyo Jumuiya hiyo itashirikiana nao kuhakikisha wanapata maendeleo zaidi.

Katika mkutano huo Chatanda ameibuka kidedea kwa kupata kura 527 za ndio zilizopigwa na wajumbe wa mkutano huo mkuu wa kumi wa UWT.

Mwenyekiti aliyemaliza muda wake, Dkt Gaudentia Kabaka amepata kura 219.

Mkutano huo mkuu wa kumi wa UWT pia umemchagua Zainabu Shomary kuwa Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa.