Neymar kuukosa mchezo dhidi ya Uswisi

0
515
Soccer Football - FIFA World Cup Qatar 2022 - Group G - Brazil v Serbia - Lusail Stadium, Lusail, Qatar - November 24, 2022 Brazil's Neymar is pictured after the match REUTERS/Molly Darlington

Mchezaji tegemeo wa Brazil, Neymar Jr ataukosa mchezo dhidi ya Uswisi kufuatia majeraha ya kifundo cha mguu aliyopata jana katika mchezo dhidi ya Serbia.

Rodrigo Lasmar, daktari wa mabingwa mara tano wa dunia amesema wanaamini nyota huyo wa PSG atakuwa mzima kushiriki katika michezo mingine ya Kombe la Dunia.

Neymar ambaye alitolewa dakika ya 80, na nafasi yake kuchukuliwa na winga wa Manchester United, Antony dos Santos, alichezewa rafu mara tisa, ikiwa ni idadi kubwa zaidi ya rafu kwa mchezaji mmoja katika mechi moja ya Kombe la Dunia 2022.

Gabriel Jesus, Antony au Gabriel Martinelli, mmoja wao atachukua nafasi ya Neymar katika kikosi cha miamba hiyo kutoka Amerika ya Kusini.

Wakati hayo yakiwa upande wa ushambuliaji, Kocha wa Brazil anabaki njia panda kufuatia beki wa kulia, Danilo da Silva naye kuwa majeruhi.

Mkongwe Dani Alves ambaye sasa anakipiga nchini Mexico anatarajiwa kuziba nafasi hiyo