Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao

0
69

Tanzania kupitia Shirika la Posta Tanzania imesaini makubaliano ya kibiashara na Shirika la Posta la Oman katika biashara mtandao.

Lengo la makubaliano hayo ni kupanua wigo wa kimataifa wa biashara mtandao, huku ikiiwezesha Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Hatua hiyo inafuatia kusainiwa kwa makubaliano ya awali mwezi Mei mwaka huu baina Shirika la Posta Tanzania na Shirika la Posta la Oman, yaliyolenga kukuza biashara za posta kupitia ushirikiano uliopo baina ya mashirika hayo.

Hatua hii ya pili ya makubaliano inalenga kukuza biashara mtandao nchini na kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha biashara mtandao kwa ukanda wa Afrika Mashariki.

Kupitia makubaliano hayo, upembuzi yakinifu sasa utafanywa ili kutoa mwelekeo wa kimkakati wa namna ya utekelezaji wa mradi huo na mikakati ya uwekezaji Tanzania kupitia Shirika la Posta.