Fedha zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kwa taasisi ya Doris Mollel, pamoja na mambo mengine zitatumika kujenga wodi ya kulea watoto Njiti wilayani Kwimba mkoani Mwanza.
Taasisi hiyo imepanga kutumia shilingi milioni 20 kati ya shilingi million 70 zilizotolewa na Rais Samia Suluhu Hassan kusaidia watoto hao Njiti.
Doris Mollel ambaye ni mwanzilishi wa taasisi hiyo ya Doris Mollel, ametembelea hospitali ya wilaya ya Kwimba kuangalia eneo itakapojengwa wodi maalum kwa ajili ya watoto Njiti na kueleza azma ya taasisi hiyo ya kusaidia watoto wanaozaliwa kabla ya wakati.
Katibu Tawala wa mkoa wa Mwanza, Balandya Mayuganya amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuchangia fedha hizo ambazo zitaisaidia wilaya ya Kwimba kuwa na uwezo wa kuwahudumia watoto Njiti.