Real Madrid yaibuka na ushindi dhidi ya Levanter

2
814

Timu ya Real Madrid imeibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Levanter katika Ligi Kuu ya Hispania.

Magoli mawili ya Real Madrid yamefungwa na wachezaji Karim Benzima na Gareth Bale kwa mikwaju ya penati.

Kwa ushindi huo, Real Madrid inafikisha alama 48 ikiwa nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi, ikitofautiana alama nane na Barcelona wanaoongoza ligi kwa kuwa na alama 57.

Athletico Madrid wao wanaendelea kushikilia nafasi ya pili kwa kufikisha alama 50 baada ya kuichapa timu ya Villareal magoli mawili kwa moja.

Magoli ya Atletico  Madrid yamefungwa na Alvaro Morata na Saul Niguez.

Katika mchezo mwingine, timu ya Leganes imetoka sare ya kufungana goli moja kwa moja na Valencia.

2 COMMENTS

Comments are closed.