Ukatili wa kijinsia Manyara wamkera Rais Samia

0
111

Rais Samia Suluhu Hassan ameiagiza Idara ya Maendeleo ya Jamii mkoani Manyara kutoa elimu ya kutosha, ili kubadili takwimu mbaya za vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani humo.

Amesema ripoti aliyopatiwa kuhusu vitendo vya ukatili wa kijinsia mkoani Manyara hairidhishi, hivyo jitihada zinahitajika kumaliza ukatili huo.

“Kwa ujumla mkoa huu wa Manyara una kesi 3,641 za ukatili wa kijinsia, lakusikitisha zaidi kesi nyingi kama 792 ni mashambulio ya kimwili.” amesema Rais Samia na kuongeza kuwa

“Kesi 708 ni kesi za unyanyasaji wa watoto kingono, sio kijinsia. Hii si rekodi nzuri wala si sifa kwa mkoa wetu.”

Rais Samia ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na wananchi wa mkoa wa Manyara uliofanyika katika uwanja wa Kwaraa, Babati.

Rais Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara yake ya siku mbili mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine amezindua mradi wa vihenge na maghala ya kuhifadhi nafaka na kuzindua barabara yenye urefu wa kilomita 8.1 Babati Mjini.