Mbeya City kuikabili Simba leo

0
55

Ligi Kuu ya soka ya NBC inaendelea hii leo kwa michezo miwili kupigwa katika viwanja viwili tofauti hapa nchini.

Katika uwanja wa Sokione, Mkoani Mbeya wenyeji Mbeya City ‘’Wana Koma Kumwanya” wanawakaribisha Wekundu wa Msimbazi katika mchezo ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Mchezo mwingine utapigwa katika Dimba la Liti Mkoani Singida ambapo wenyeji Singida Big Stars watawaalika wakusanya ushuru wa Kinondoni KMC ikiwa ni mchezo wa kuhitimisha mzunguko wa 13 wa ligi kuu ya NBC.

Mchezo kati ya Mbeya City na Simba utakuwa ni wa aina yake kutokana na kila timu kuwa katika kiwango bora kwa sasa huku Simba ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mchezo wa msimu uliopita ambao ulipigwa Mkoani Mbeya.

Simba ipo katika nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na alama 27 baada ya kushuka dimbani mara 12 huku Mbeya City ikiwa katika nafasi ya tano baada ya kushuka Dimbani mara 12 na kujikusanyia alama 18.