Hernandez nje kikosi cha Ufaransa

0
109

Kambi ya mabingwa watetezi wa Kombe la Dunia Ufaransa imeendelea kupata pigo baada ya mlinzi wake wa kushoto Lucas Hernandez kuumia goti na huenda akashindwa kurejea uwanjani katika kipindi kifupi.

Hernandez (26) ambaye pia ni mlinzi wa kushoto wa Bayern Munich aliondolewa uwanjani baada kuumia goti katika mchezo ambao mabingwa wa Dunia Ufaransa waliiadhibu Australia Mabao 4-1.

Hernandez anaongeza idadi ya wachezaji nyota wa Ufaransa ambao wameumia na wanakosa michuano ya kombe la Dunia mwaka huu akiwemo Mshindi wa Tuzo ya Ballon D’or Karim Benzema, Ng’olo Kante na Paul Pogba.

“Nampa pole sana Lucas (Hernandez) na kwa kweli tumepata pigo lingine katika kikosi chetu” amesema Didier Deschamps kocha wa Ufaransa.

“Tumempoteza mchezaji mzuri, Lucas ni tishio na sina mashaka atarejea tena kuipigania taifa lake”- ameongeza Deschamps