Chandi kuunganisha chama na serikali

0
64

Mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Mara, Patrick Chandi ameahidi kukiunganisha chama na serikali ndani ya mkoa huo ili kuweza kutekeleza ilani ya CCM na kuwaletea wananchi maendeleo.

Chandi ameyasema hayo wakati akitoa shukrani kwa wajumbe wa mkutano mkuu mara baada ya kushinda kiti hicho ambapo amesema ili kuleta ufanisi wa utendaji pamoja na maendeleo ni lazima chama na Serikali vifanye kazi pamoja.