Wachezaji wa Iran wagoma kuimba wimbo wa Taifa

0
129

Wachezaji wa Timu ya Taifa ya Iran hawakuimba wimbo wa Taifa lao wakati wa mchezo wao na England ikiwa ni ishara ya kuunga mkono maandamano dhidi ya serikali nchini mwao.

Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo walishikilia mabango yenye jumbe mbalimbali zilizoandikwa Wanawake, Maisha, na Uhuru.

Kumekuwa na maandamano ambayo yanasambaratishwa na Serikali yaliyotokana na kifo cha kijana Mahsa Amini, aliyefariki akiwa mikononi mwa polisi.

Watetezi wa haki za binadamu wamesema kuwa zaidi ya waandamanaji 400 wameuawa huku wengine 16,800 wakishikiliwa na vyombo vya ulinzi.

Akizungumza kabla ya mchezo huo, Nahodha wa Iran, Ehsan Hajsafi amesema kuwa wachezaji wanasikitika na wote waliofariki.

Mchezo huo umemalizika kwa Iran kufungwa magoli 6-2.