CCM yafuta uchaguzi wa UVCCM Simiyu

0
55

Chama Cha Mapinduzi (CCM), kimefuta uchaguzi wa viongozi wa Umoja wa Vijana wa chama hicho (UVCCM) mkoani Simiyu kutokana na tuhuma za ukikwaji wa taratibu.

CCM pia imefuta uchaguzi wa Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa kwa mikoa ya Mbeya na Arusha kwa tuhuma za ukiukwaji wa maadili pamoja na rushwa.

Katibu Mkuu wa CCM Taifa Daniel Chongolo ameyasema hayo wakati wa mkutano wake na waandishi wa habari.

Aidha CCM Inafanya uchunguzi wa tukio la mwanachama kukimbia na sanduku la kura wakati wa uchaguzi uliofanyika mkoa wa Mjini Magharibi, Zanzibar.