Pombe viwanjani marufuku Qatar

0
985

Uuzaji wa pombe umepigwa marufuku katika viwanja vyote vitakavyotumika wakati wa michuano ya Kombe la FIFA la dunia itakayoanza tarehe 20 mwezi huu nchini Qatar.

Awali ulitangazwa utaratibu maalum wa uuzaji pombe katika maeneo ya viwanja katika nchi hiyo ambapo uuzaji wa bia za Bud Zero zisizo na vilevi ukiruhusiwa.

Tangazo hilo jipya la Qatar limetolewa hii leo, ikiwa ni siku mbili tu kabla ya kuanza kutimua vumbi kwa michuano hiyo ambapo Qatar itashuka dimbani kumenyana na Ecuador.