Uwanja wa Ihefu FC wafungiwa

0
217

Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeufungia uwanja wa Highland Estates uliopo Mbarali mkoani Mbeya kutumika katika michezo ya ligi.

Mamlaka hiyo imesema kuwa uwanja huo unakosa vigezo vya kikanuni na sheria za mpira wa miguu. Eneo la kuchezea (pitch) la uwanja halina majani ya kutosha na yaliyopo hayajakatwa kwa usawa, hivyo kuufanya uwanja kutokuwa salama kwa watumiaji pamoja na kupunguza ubora wa mchezo.

Kufuatia uamuzi huo, bodi imeitaka Ihefu FC ambayo inatumia uwanja huo kutumia uwanja wa Sokoine jijini Mbeya hadi hapo uwanja wao utakapofunguliwa baada ya marekebisho.

Ihefu FC ipo nafasi ya mwisho katika msimamo wa Ligi ya NBC ikiwa na alama 5 baada kushuka dimbani mara 11.