Doris Mollel kuisaidia Uganda kuokoa watoto Njiti

0
138

Mkurugenzi wa taasisi ya Doris Mollel , Doris Mollel amealikwa na wizara ya Afya nchini Uganda kwa lengo la kusaidia kuwapatia uzoefu wataalamu wake wa kukabiliana na vifo vya watoto Njiti nchini humo.

Mollel amekutana na wakurugenzi wa wizara ya Afya nchini Uganda na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Kawala Dorothy Ajiong baada ya kufanya ziara katika hospitali hiyo na kujionea utoaji huduma ya Mama na Mtoto.

Doris Mollel yupo nchini Uganda kwa mwaliko maalum na anatarajiwa kuwa mgeni wa heshima kwenye maadhimisho ya kitaifa ya Siku ya Mtoto Njiti Duniani.