Mabingwa watetezi wa michuano ya Kombe la FIFA la Dunia Ufaransa wamewasili nchini Qatar kwa ajili ya kutetea ubingwa wao waliouchukua mwaka 2018.
Miamba hiyo ya Dunia imewasili usiku wa kuamkia leo katika mji Mkuu wa Qatar, Doha ikiwa na nyota wake wote pamoja na mchezaji bora wa Dunia Karim Benzema.
Kikosi hicho kinachonolewa na Nahodha wa zamani wa Ufaransa Didier Deschamps kinapewa nafasi ya kufanya vyema katika michuano hiyo ingawa haitakuwa rahisi kutokana na maandalizi ya mataifa mengi yanayoshiriki michuano hiyo.
Ufaransa ipo katika kundi D pamoja na Tunisia, Australia na Denmark