Wakosoaji wamjia juu Rais Weah

0
120

Waziri wa Fedha wa Liberia, Samuel Tweah amesema, Rais George Weah wa nchi hiyo anastahili posho ya dola elfu mbili za kimarekani kwa siku (takribani shilingi 4,660,000 za kitanzania) wakati wa safari yake ya nje ya nchi iliyoanza tarehe 1 mwezi huu hadi tarehe 23 mwezi huu.

Siku hizo zinajumuisha kukaa nchini Qatar kwa muda wa siku 9 kutazama mechi za Kombe la Dunia.

Wakosoaji wanasema kumtunuku Rais Weah kiasi kikubwa kama hicho kwa cha fedha kwa siku ni kinyume na ahadi yake ya kupunguza matumizi ya fedha za umma kwa ajili ya ajenda yake ya kuwasaidia watu wa hali ya chini.

Taarifa zaidi zinasema Rais huyo wa Liberia anapanga kupita Qatar ili kumuangalia mtoto wake ambaye ni mzaliwa wa Marekani akicheza mechi ya Kombe la Dunia dhidi ya Wales.