Yanga yarejea kileleni

0
93

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya soka ya NBC Klabu ya soka ya Yanga imerejea kileleni baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1 kwa bila dhidi ya walima miwa wa Kagera, Kagera Sugar.

Bao la Yanga limefungwa dakika ya 18 na mchezaji kinda Clement Mziza baada ya majalo safi ya Feisal Salum.

Kagera Sugar itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kupoteza nafasi ya kusawazisha baada ya kiungo Mshambuliaji wake Eric Mwijage kupiga mkwaju wa penati uliookolewa na mlinda lango wa Yanga Djigui Diarra.