Nape: Tumuunge mkono Rais Samia

0
1003

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye ametoa wito kwa wasanii nchini kuendelea kumuunga mkono Rais Samia Suluhu Hassan katika kupeleka mbele gurudumu la maendeleo na wasanii kuweza kunufaika na kazi zao.

Nape amezungumza hayo kwenye tamasha la Suluhu lililoandaliwa na Msanii Jay Dee akishirikiana na Msanii Rama Dee linalofanyika katika ukumbi wa Hyatt jijini Dar es Salaam.

Wakati huo msanii Lady Jaydee ametumia tamasha hilo kuzindua taasisi aliyoipa jina la ‘Binti Foundation’ itakayohusika kuwainua na kumkomboa mwanamke.

Mbali na Jay Dee na Rama Dee wasanii wengine kama vile Patricia Hillary, TID, Man Dojo na Domokaya wamealikwa kutoa burudani kwenye tamasha hilo.