Mkwanja wa Kombe la Dunia 2022

0
225

MKWANJA WA KOMBE  LA DUNIA

Hii ndiyo  michuano yenye thamani zaidi uliwenguni, FIFA wametenga bajeti ya dola bilioni 4.6 ambapo haki za matangazo ya michuano hii zitazalisha dola bilioni 2.6

Zawadi kwa ajili ya washindi zimeongezeka kutoka dola milioni 358 mpaka Kufikia  dola milioni 440 kukiwa na ongezeko la dola milioni  40 Kutoka michuano ya mwaka 2018

Bingwa wa mashindano haya atajizolea dola milioni 42  ambayo ni sawa na shilingi bilioni 96.6 kukiwa na ongezeko la dola milioni 4 kutoka mwaka 2018.

Timu itakayomaliza nafasi ya  pili itabeba dola milioni 30 (69b Tsh) mshindi wa tatu atapata kitita cha dola bilioni 27 (62.1b Tsh) huku nafasi ya nne akijipatia  dola milioni 25 (57.5b Tsh)

Timu zitakazofika hatua ya robo fainali zitajikusanyia dola bilioni 17 (39.1b Tsh) na watakaoishia hatua ya 16 bora watajizolea dola milioni 13 sawa na shilingi bilioni (29.9b Tsh)

Fifa pia wanatoa kiasi cha dola milioni 10.5 (24.1b Tsh) kwa kila timu shiriki kwa ajili ya maandalizi ya awali ya michuano hiyo ambapo tayari awamu ya kwanza imekwisha tolewa.

Bado siku 8, kaa tayari kutazama na kusikiliza Fainali za Kombe la Dunia kupitia TBC buuree kuanzia Novemba 20 – Disemba 18.