Kitabu kilichoandikwa na wasomi 45 chazinduliwa

0
117

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Profesa Adolf Mkenda amesema kwa sasa serikali ipo katika hatua nzuri ya kukamilisha mchakato wa kuboreaha mfumo wa elimu na mitaala.

Waziri Mkenda ametoa kauli hiyo jijini Dodoma wakati akizindua kitabu kilichopewa jina la CONTINUTY WITH VISION THE ROAD MAP TO SUCCESS FOR PRESIDENT SAMIA SULUHU HASSANĀ  kilichoandikwa na wasomi mbalimbali nchini.

Kitabu hicho chenye kurasa 624 na sura 29, kimeandikwa na wanazuoni 45 akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) Dkt. Ayub Rioba Chacha, Dkt. Joviter Katabaro na Dkt. Shauri Timothy na kupitiwa na wahariri watatu.