Darasa la Kiswahili lazinduliwa Malawi

0
130

Malawi imezindua darasa la kwanza la lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Hebron.

Darasa hilo limezinduliwa na waziri wa Elimu wa Malawi, Agnes Nyalonje ambaye amesema uanzishwaji wa darasa hilo ni kati ya ushirikiano muhimu kwa nchi za Tanzania na nchi hiyo.

“Ushirikiano huu ni muhimu na wenye thamani ,tutauenzi na kuhakikisha Kiswahili kinakua kwa kasi nchini kwetu.” amesema waziri Nyalonje

Kwa upande wake Balozi wa Tanzania nchini Malawi, Humphrey Polepole amesema kuanzishwa kwa darasa hilo ni muendelezo wa uhusiano mzuri wa nchi hizo mbili na kwamba atasimamia utekelezaji katika kuhakikisha Kiswahili kinakua .

Ameongeza kuwa anaamini watu wengi nchini Malawi wataweza kujua kwa haraka lugha ya kiswahili ambayo itawasaidia katika nyanja mbalimbali.

Walimu wa darasa hilo la lugha ya kiswahili nchini Malawi watafundisha kwa muda wa wiki moja na wametoka Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA).