Mchezo wa Ligi kuu ya soka ya NBC baina ya walima alizeti wa Singida na Simba SC umemalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana bao moja kwa moja.
Singida Big Stars walikua wa kwanza kupata bao katika dakika ya 11 ya mchezo kupitia kwa kiungo Mshambuliaji wake Deus Kaseke.
Bao hilo la Singida Big Stars lilidumu mpaka mapumziko.
Kipindi cha pili Simba walikuja kivingine na mabadiliko ya kumuingiza Peter Banda yaliwasaidia kusawazisha bao hilo katika dakika ya 58.
Licha ya kumiliki mpira kwa muda mrefu lakini haikuwasaidia Simba kuibuka na ushindi katika mchezo huo wa leo ambapo mpaka kipyenga cha Mwamuzi Elly Sasi kinahitimisha mchezo huo matokeo yalikua bao moja kwa moja.
Kwa matokeo hayo Simba wanasalia katika nafasi ya pili ya msimamo wa Ligi hiyo kwa kukusanya alama 18 baada ya kushuka dimbani mara 9 huku Singida Big Stars wao wakisalia nafasi ya tatu kwa kuwa na alama 18 wakiwa wamecheza Michezo 10.