MANUSURA : NDANI YA DAKIKA MOJA MAJI YALIJAA KWENYE NDEGE

0
228

Nickson Jackson ambaye ni miongoni mwa watu 24 waliookolewa wakiwa hai kwenye ajali ya ndege iliyotokea mkoani Kagera amesema, ndani ya dakika moja baada ya ndege hiyo kupata ajali maji yalianza kujaa ndani na hivyo kuwafanya watu waliokuwamo ndani kuanza kutafuta njia za kujiokoa.

Nickson alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam ilipofanyika shughuli ya kuaga miili mitano kati ya 19 ya watu waliofariki dunia katika ajali hiyo ya ndege katika ziwa Victoria.

Video nzima ipo YouTube channel yetu ya TBCOnline