Msemaji Mkuu wa Serikali Gerson Msigwa amesema ni majeruhi mmoja tu kati ya 26 wa ajali ya ndege ya Precision iliyotokea tarehe 6 mwezi huu mkoani Kagera ndiye anayeendelea kupatiwa matibabu hospitalini baada ya wengine kuruhusiwa.
“Waliokolewa watu 26 lakini waliokwenda hospitali ni 24, hawa wawili hawakupata majeraha makubwa kwa hiyo hawakufikishwa hospitali, kati ya hawa majeruhiu waliolazwa Hospitali, mmoja tu ndio yupo hospitali na wengine 23 wameruhusiwa.” amesema Msemaji Mkuu wa Serikali
Alikuwa akizungumza na waandishi wa habari mjini Bukoba, siku moja baada ya kutokea kwa ajali hiyo ya ndege katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19.