Kujifunza lugha ngumu kwa njia rahisi

0
103

Ni matamanio kwa kila mtu kufahamu lugha zaidi ya moja, lakini maswali ya kujiuliza ni lugha gani?. Lakini pia zipo lugha ambazo zinaaminika ni ngumu kujifunza ikiwemo kichina.

Mkurugenzi wa Taasisi ya Confucius Chuo Kikuu Dar es Salaam Profesa Aldin Mutembei amesema zipo njia rahisi za kujifunza lugha ambazo zinaonekana ni ngumu kuzizungumza hususani kichina.

Profesa Mutembei ameongeza kuwa lugha ya kichina inajihusisha zaidi na michoro tofauti na lugha nyingine ambazo ni herufi, hivyo mtu anayejifundisha lugha ya kichina anaanza kwa kufundishwa michoro ya kichina.

“Kwenye lugha ya kichina hufundishwa kuchora tu misamiati yao bali unafundishwa utamaduni wao, kwa hiyo ukisema ujifunze kichina maana yake unajifunza utamaduni wa China, ndio maana unaona watu wanaokwenda kusoma China kabla ya kusoma masomo waliyoyafuata wanafundishwa utamaduni wa China ikiwemo kuchora lugha ya kichina.” amesema Profesa Mutembei

Kuhusu wingi wa maneno, Profesa Mutembei amesema mchoro mmoja wa kichina unaweza kumaanisha taarifa zaidi ya moja ambayo inaweza kukaa kwenye neno moja tu.

“Mfano neno la kiswahili Nakuja, Nilikuja ama Nitakuja hapo unabadilisha herufi, lakini kwenye lugha ya kichina mchoro huo huo mmoja unaweza kuakisi maneno yote hayo na mtu kufahamu kuwa ulikusudia kufikisha taarifa gani.”ameongeza Profesa Mutembei

Je, unapenda kujifunza lugha gani?.