Kuiona Azam FC Chamazi ni bure

0
134

Klabu ya soka ya Azam FC imetangaza kuwa kuanzia sasa mechi zao zote zilizobaki za msimu huu, watakazocheza katika uwanja wao wa nyumabani Azam Complex, Chamazi hakutakuwa na kiingilio zaidi ya shabiki atatakiwa kuvaa jezi yoyote ya Azam FC.

Jumatano hii, Azam FC watashuka dimbani katika dimba la Azam Complex kuvaana na Dodoma jiji FC katika mechi za muendelezo wa Ligi Kuu ya NBC, kuanzia Saa 1:00 Usiku.

Mpaka sasa Azam FC ipo nafasi ya 3 katika msimamo wa Ligi Kuu ya NBC baada ya kushuka dimbani mara 3 na kujikusanyia alama 17.