Aliyejiunga na IS ataka kurejea Marekani

0
890

Mwanamke mmoja raia wa Marekani aliyetoroka nchini mwake na kwenda nchini Syria kujiunga na Wanamgambo wa IS miaka kadhaa iliyopita, amesema kuwa anajutia kufanya kitendo hicho na hivi sasa anataka kurejea nyumbani.

Mwanasheria wa  anayemtetea mwanamke huyo, amesema kuwa mteja wake Hoda Muthana alizaliwa katika mji wa New Jersey, hivyo ni raia wa Marekani  kwa kuzaliwa na ana haki zote za kurejea nyumbani.

Hata hivyo Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani, – Mike Pompeo  amesema kuwa wanamke huyo haruhusiwi kurejea Marekani kwani amepoteza haki yake ya kuwa raia wa  nchi hiyo baada ya kuondoka na kuamua kujiunga na Wanamgambo hao wa IS.

Hoda mwenye umri wa miaka 24 hivi sasa aliondoka nchini Marekani kwenda nchini Syria akiwa na umri wa miaka Ishirini, na kusema kuwa anakwenda nchini Uturuki kujiunga na Chuo Kikuu.