Ruvu Shooting Vs Tanzania Prisons kukiwasha

0
127

Ligi kuu ya soka ya NBC inaendelea hii leo kwa mchezo mmoja utakaopigwa kwenye uwanja wa uhuru, mkoani Dar es salaam ambapo maafande wa Ruvu Shooting watawaalika maafande wenzao wa Magereza Tanzania Prisons.

Mchezo huo wa mzunguko wa 11 utashuhudia Ruvu shooting ikijaribu kujiweka sawa katika msimamo wa ligi huku Prisons akitafuta namna ya kukwea nafasi ya tatu katika msimamo wa ligi hiyo.

Ruvu shooting inayonolewa na Charles Boniface Mkwasa ipo nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ikiwa na alama 10 baada ya kushuka dimbani mara 9 huku Tanzania Prisons yenyewe ikiwa katika nafasi ya 7 baada ya kujikusanyia alama 13 katika michezo 9 iliyocheza.

Mpaka sasa mabingwa watetezi wa ligi hiyo klabu ya soka ya Yanga inashikilia usukani baada ya kujikusanyia alama 20 ikifuatiwa na Simba yenye alama 17 na Azam Fc ni ya tatu ikiwa na alama 17