Kijana aliyeokoa watu kwenye ndege azawadiwa

0
290

Mkuu wa mkoa wa Kagera, Albert Chalamila amempatia kijana
Majaliwa Jackson shilingi milioni moja ikiwa ni kumshukuru kufuatia kitendo chake cha kishujaa baada ya kuwaokoa watu 24 wakiwa hai kutoka ndani ya ndege ya Precision iliyopata ajali hapo jana katika ziwa Victoria.

Chalamila amempatia Majaliwa fedha hizo wakati wa shughuli ya kuaga miili ya watu 19 waliofariki dunia katika ajali hiyo, shughuli iliyoongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Mkuu huyo wa mkoa wa Kagera amesema, kama si kitendo kilichofanywa na kijana huyo, idadi ya watu waliofariki dunia huenda ingekuwa kubwa zaidi.

Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo kijana huyo ambaye ni mvuvi, alitumia kasia kufungua mlango wa ndege hiyo ya Precision na hivyo kufanikisha kutoka ndani ya ndege watu 24 wakiwa hai.