Waliofariki dunia Bukoba kuagwa leo

0
214

Miili ya watu 19 waliofariki dunia katika ajali ya ndege ya Shirika la ndege la Precision iliyotokea hapo jana mkoani Kagera inaagwa asubuhi hii, katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba.

Shughuli ya kuaga miili hiyo itaongozwa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye tayari yupo mkoani Kagera kuanzia hapo jana.

Ajali hiyo imetokea katika ziwa Victoria wakati ndege hiyo ikiwa katika safari zake za kawaida kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba.

Ilipata ajali takribani mita mia moja kabla ya kutua katika uwanja huo wa ndege wa Bukoba.