Precision yatangaza vituo vya kupata taarifa

0
141

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la ndege la Precision Air Patrick Mwanri, ametangaza vituo viwili kwa ajili ya kusaidia kupata taarifa familia za abiria waliokuwa wakisafiri na ndege ya shirika hilo ambayo imepata ajali mapema hii leo mkoani Kagera.

Amewaambia waandishi wa habari mkoani Dar es Salaam kuwa kituo kimoja kipo katika hotel ya EACT Bukoba, na kwa Dar es Salaam kituo kipo eneo la Vingunguti katika hotel ya Blue Sapphire.

Ndege hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea Bukoba imepata ajali katika ziwa Victoria ikiwa na watu 43 ndani ambao ni abiria pamoja na wafanyakazi wa ndege hiyo.