Nyota waliotwaa Kombe la Dunia Kwa rekodi

0
331

Nyota walioshinda Kombe la Dunia wakiwa kama wachezaji na baadae kushinda wakiwa kama makocha wa nchi zao.

Franz Beckenbauer (Ujerumani) alishinda Kombe la Dunia akiwa Mchezaji mwaka 1974 na kisha akashinda akiwa kocha mwaka 1990.

Mario Zaggalo (Brazil) alishinda Kombe la Dunia mwaka 1958 na 1962 akiwa kama Mchezaji na kisha akashinda akiwa kocha mwaka 1970.

Didier Deschamps (Ufaransa) alishinda mwaka 1998 kama mchezaji na miaka 20 baadae mwaka 2018 akashinda akiwa kama kocha.

Bado siku 15, kaa tayari kutazama na kusikiliza Fainali za Kombe la Dunia kupitia TBC buuree kuanzia Novemba 20 – Disemba 18.