TEWW, Baraza la Ushindani wapata mabosi wapya

0
1106

Rais John Magufuli amemteua Dkt Michael Ng’umbi kuwa Mkurugenzi wa Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW).

Kabla ya uteuzi huo Dkt Ng’umbi alikuwa Mhadhiri Mwandamizi wa Kitivo cha Elimu cha Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

Dkt Ng’umbi anachukua nafasi ya Dkt Fidelice Mafumiko ambaye ameteuliwa kuwa Mkemia Mkuu wa Serikali.

Wakati huohuo, Rais Magufuli amemteua Jaji Stephen Magoiga kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Ushindani.

Jaji Magoiga anachukua nafasi ya Jaji Barke Sehel ambaye ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.

Taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa viongozi hao umeanza Februari 19 mwaka huu.