Katavi ina Ghorofa 70 tu

0
255

Tanzania ina jumla ya majengo ya ghorofa 68,724 kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022.

Katavi ndio mkoa wenye ghorofa chache zaidi Tanzania, ukiwa na ghorofa 70. Mikoa mingine inayofuatia kwa kuwa na idadi ndogo ya ghorofa ni;

  1. Simiyu: 138
  2. Rukwa: 173
  3. Songwe: 174
  4. Kaskazini Pemba: 222

Kwa upande wa mikoa inayoongoza, Dar es Salaam unashika nafasi ya kwanza ukiwa na ghorofa 32,219. Mikoa inayofuatia ni;

  1. Arusha: 7,180
  2. Mjini Magharibi: 5,453
  3. Tanga: 4,282
  4. Kilimanjaro: 3,540